Kiswahili Language Version of "Top 10 Myths About Civil Society Participation at ICANN"

Brenden Kuerbis bkuerbis at INTERNETGOVERNANCE.ORG
Tue Sep 15 21:29:24 CEST 2009


Alex,

This is fantastic!  Did you or Grace post it to the website blog?  Any ideas
on how best to ensure some of those 120 million Kiswahili speakers in East
Africa see this wonderful translation?

Thanks!

---------------------------------------
Brenden Kuerbis
Internet Governance Project
http://internetgovernance.org


2009/9/15 Alex Gakuru <gakuru at gmail.com>

> Hi Robin, all,
>
> Grace Muting'u has kindly translated the document into Kiswahili
> (spoken by at least 120 million people in East African Community
> member countries alone).
>
> Asante (Thanks) Grace.
>
> Regards,
>
> Alex
>
> ---begins----
> “Porojo Kumi maarufu zaidi  kuhusu uhusikaji wa mashirika ya shirika
> la ICANN”, na NCUC
>
> 21 Agosti 2009
>
> _____________________________________________________________________________
> Porojo ya Kwanza
>
> “Masirika ya kijamii hayatahusika kwenya ICANN chini ya mpango
> uliopendekezwa na NCUC.”
>
> Uwongo: Wafanyakazi wa ICANN na wengine wanadai kwamba
> mashirika  ya  kijamii hukatwa tamaa yasijihusishe na ICANN
> kwa vile mpango uliopendekezwa na ICANN hauhakikishi kwamba
> viti katika Kamati ya GNSO vitagawiwa maeneo au washikadau wote.
>
> Ukweli wa mambo ni kwamba uanachama wa NCUC unawakilisha
> mashirika 143 yasiyo ya kibiashara pamoja na watu binafsi. Tangu
> mwaka 2008 uanachama wa NCUC umeongezeka kwa zaidi ya 215%
> - hii ni kwa mujibu wa mwito wa mashirika ya kijamii. Hakuna shirika
> hata moja lisilo la kibiashara lililotoa maoni kwamba kuwepo tu kwa
> viti vya maeneo katika Kamati ya GNSO ndipo kungewafanya kushiriki
> kwenye ICANN. Katika mashirika yaliyotoa maoni yao, hakuna
> lilisosema ya kwamba lingeshiriki kwenye ICANN sharti katiba ya
> NSCG ingewahakikishia kiti kwenye Kamati ya GNSO.
>
> Porojo ya Pili
>
> “Wengi zaidi kutoka mashirika ya kijamii watashiriki kwenye ICANN
> Bodi itakapoingilia”
>
> Picha ya kweli: Kulazimisha kwa Bodi kwa katiba yake au kutosikiliza
> kwa Bodi kwa vikundi vya mashirika ya kijamii kutaonekana kama
> kukataliwa kwa maoni ya vile vikundi vingi vilivyoonelea kwamba ni hii
> ni dhuluma dhidi ya mashirika ya kijamii. Sifa ya ICANN kati ya
> mashirika yasiyo ya kibiashara itaharibika kabisa hatua mwafaka
> isipochukuliwa au suluhu kupatikana. Hata kama vitendo hivyo
> vingekubalika, matokeo  kamili kwa wafanya kazi na kwa katiba
> ya NCSG itakuwa kuvinyima nguvu vikundi visivyo vya kibiashara
> na kuvifanya hata visipende kushiriki. Kuteuliwa kwa waakilishi na
> Bodi hufurutisha  vikundi visivyo vya kibiashara na watu binafsi.
> Isitoshe, SIC inayowakilisha maeneo au washika dau wote inahitaji
> fedha nyingi sana ambayo mashirika mengi yasiyo ya kibiashara
> hayawezi kusimamilia. Pia, mpangilio huo utaleta mgawanyiko kati
> ya vikundi huku vikipigania wanachama na kura. Vikundi vingi visivyo
> vya kibiashara havitaweza kuingia ICANN GNSO chini ya mpango huo.
>
> Porojo ya Tatu
>
> Kuwepo kwa upinzani kunaweza kupuuzwa tu kama “kampeni ya
> uandikaji barua”
>
> Hii ni shutma isiyo ya kweli: Upinzani mkali wa mashirika ya kijamii
> kwa katiba ya SIC ulitokea si mara moja bali mara mbili. Pia, kulikuwa
> na ongezeko kubwa la wanachama wa NCUC lililotokana na kutopendezwa
> kwa jamii yote kwa jumla na vitendo vya wafanyakazi pamoja na Bodi.
> Kujaribu kupunguza ushiriki wa mashirika ya kijamii hakutafanikiwa na
> kunaonyesha upotovu huu wa hali ya juu. ICANN inahitajika kuwa na
> nyakati za maoni ya umma kwa maana ni lazima isikize na kujibu
> maswala ya jamii. Maoni ya umma hutokana na kuwepo kwa mawasiliano
> na mazungumzo kuhusu hata maswala tata, hata kama ni  miito ya
> kuchukua hatua. Hakuna mpango au sheria inayoipa ICANN au
> wafanyakazi wake uwezo wa kuamua kutotilia maanani au kupuuza
> vikundi karibu vyote vilivyoonyesha kutaka kushiriki kwenye marekebisho
> ya GNSO, eti kwa sababu wamewashutumu wafanyakazi wa ICANN.
>
> Jaribio la ICANN la kutaja maoni haya ya muhimu kama “kampeni ya
> uandikaji barua” inapuuza ushiriki wa siku zijazo na imani katika
> mipango ya ICANN ya kuhusisha umma.
>
> Porojo ya Nne
>
> "Mashirika ya kijamii yamegawanyika kuhusu swala la katiba ya NCSG."
>
> Si Kweli. Hakujawahi kuwa na maoni ya umma yaliyoegemea upande mmoja
> kama haya katika historia ya ICANN. Hata kama wafanyikazi wa ICANN
> wanaiambia Bodi kwamba mashirika ya kijamii yamegawanyika, maoni zaidi
> yanakataa katiba iliyopendekezwa na ICANN na kuiunga mkono
> iliyopendekezwa na NCUC. Wanabodi wanaotegemea habari kutoka kwa
> wafanyikazi wa ICANN pekee wanaweza kuamini kwamba mashirika ya
> kijamii yamegawanyika , lakini wanabodi ambao wanesoma maoni ya umma
> wanaweza kuona umoja wa mashirika ya kijamii katika kupinga kulazimishwa
> kufanya ICANN inavyotaka.
>
> Porojo ya Tano
>
> "Mashirika ya Kijamii yaliyoko kwa sasa hayawakilishi kamili washikadau
> wote"
>
> Si kweli kwa vyovyote. Kwa sasa, kikundi cha mashirika ya kijamii,
> kijulikanacho
> kama NCUC kina wanachama 143 ambao kati yao 73 ni mashirika yasiyo ya
> kibiashara na watu banafsi 70 kutoka nchi 48. Hili ni ongezeko la 215%
> tangu
> kanuni  ya uakilishaji wa wote ianzishwe.
>
> Ushiriki wa jamii isiyo ya kibiashara umeongezeka na kwa hivyo si haki
> kusema
> kusema kwamba NCUC haishirikishi washika dau wote bila ya kusema hivyo juu
> ya jamii zingine. Hata mwaka wa 2006, utafiti huru uliofanywa na London
> School
> of Economics ulionyesha kuwa NCUC iliwakilisha maeneo mengi zaidi na pia
> ilikuwa na watu wengi zaidi tofauti katika kamati ya GNSO wakati wowote, na
> kwamba ilibadilisha zaidi wawakilishi wake katika kamati hio ikilinganishwa
> na
> jamii zile zingine sita.
>
> Kwa upande mwingine, jamii ya wanabiashara imekuwa ikiwakilishwa na watu
> wale wale 5 kwa Kamati kwa muongo mmoja na kulipokuwa na mwito wa
> marekebisho ya GNSO, 3 kati ya wanakamati 6 wa jamii ya kibiashra
> watawakilisha Marekani.
>
> Porojo ya Sita
>
> “ALAC inapendelea mkataba uliopendekezwa na wafanyakazi wa ICANN
> kuliko ule wa mashirika ya kijamii”
>
> Uwongo: Kiongozi mmoja wa ALAC alisema kuwa anapendelea maktaba
> uliopendekezwa na wafanyikazi. Wafanyikazi walichukua msemo huo na
> kuupeleka kwa Bodi ya ICANN huku wakidai kwamba ALAC inapendelea
> mkataba uliopendekezwa na wafanyikazi wa ICANN. Kwa kweli, taarifa
> rasmi iliyotolewa na ALAC na iliyopitishwa na na ALAC ilisema kuwa
> wanachama wengi wa ALAC waliunga mkono pendekezo la “kulitenganisha
> swala la viti vya Kamati kutoka kwa maeneo ni jambo nzuri na mwelekeo
> mwema.”
>
> Porojo ya Saba
>
> "Mkataba wa NCUC utakipa kikundi kile kile kidogo viti 6 badala ya 3"
>
> Uwongo:   Kwa miezi minane iliyopita, NCUC imekuwa ikitangaza kuwa
> itajitawanya muda tu NCSG itakapoundwa. Haina maana kuwa na “jamii ya
> mashirika yasiyo ya kibiashara” na vile vile “washika dau wasio wa
> kibiashara” kwani haya ni maneno yenye maana sawa. Kwa hivyo, viongozi
> wa NCUC hawatakuwa na uwezo wa kuendesha NCSG mpya – uongozi mpya
> utachaguliwa. Chini ya mkataba, mashirika na watu wote binafsi watapiga
> kura kuchaga viti vya Kamati, na si tu wanachama wa hapo mbeleni wa
> NCUC. Masharti makali kuhusu uakilishi kutoka maeneo yote ya kijografia
> yatamaanisha kuwa wanaowania kutoka maeneo yote duniani
>  watachaguliwa hata kama hawatapata wingi wa kura.
>
> Porojo ya Nane
>
> "NCUC haitagawana viti vya Kamati na jamii zingine za mashirika yasiyo
> ya kibiashara."
>
> Si Kweli: Mkataba wa NCUC uliundwa ili kuwezesha mashirika yasiyo ya
> kibiashara kuwa na wawaniaji wao wa viti vya Kamati. Ikilinganishwa na
> uwepo na uanachama wa NCUC, jamii nyingi zenye ajenda zinazoshindana
> zitajitokeza. Kukua kwa maeneo kutoka mashinani hadi juu ni bora
> kuliko mwelekeo wa Bodi/Wafanyikazi- pia unafanana zaidi na mapedekezo
> ya BGC. Maktaba wa SIC unaelekeza uundaji wa maeneo kutoka juu na hii
> ni ngumu na inaipa Bodi uwezo uliozidi kuamua “ushirikishaji” au
>  “umuhimu” wa washiriki wapya. Kwa vile uakilishi wa maeneo unategemea
> viti vya Kamati. Viti vya Kamati vikilinganishwa na maeneo, kila eneo
> litakuwa na mivurutano kuhusu kupewa kwa viti hivi vya Kamati
>
> Porojo ya Tisa
>
> "NCUC inataka kunyakua haki ya Bodi ya kupitisha maeneo”
>
> Uwongo: Watu wanaosema hivi ni dhahiri ya kwamba hawajasoma mkataba
> uliopendekezwa na NCUC. NCUC inapendekeza kwambo Bodi iwe na uwezo wa
> kupitisha au kukataza maeneo mapya yaliyoundwa chini ya mkataba huo.
>
> Pendekezo letu ni kuwe na na mielekezo ya kufuatwa (k.m nambari ya
> wagombea) kwa kuundwa kwa maeneo mapya halafu mapendekezo
> yatumwe kwa Bodi. Dhana ilikuwa kupunguza mzigo wa uundaji wa maeneo mapya
> kwa
> wagombea na pia kwa Bodi.
>
> Mkataba uliopendekezwa na NCUC una mapendekezo rahisi sana ya kuunda
> maeneo mapya ukilinganishwa na ule wa SIC ambao utafanya uundaji wa
> maeneo mapya kuwa jambo gumu sana.
>
> Porojo ya Kumi
>
> “Azma ya kuwa na eneo ni kuwa na kiti kwenya Kamati ya  GNSO.”
>
> Uwongo:  wengine hudai kwamba viti vya Kamati ya GNSO lazima
> vilinganishwe kikamili na maeneo haswa kwa vile eneo halina maana bila
> kuhakikishiwa kiti kwenye Kamati ya GNSO. Lakini, kusema hivyo ni
> kutoelewa umuhimu wa maeneo katika GNSO mpya, ambao ni kuwapa sauti na
> namna ya kushiriki katika utengenezaji wa sera –wala si kuhakikishiwa
> kuwa na mjumbe asiye hata na mori wa kuafikiana na maeneo mengine.
>
> Viwili kati ya vikundi vitatu vya washikadau (Registries and Registrars)
> vilipitisha mwelekeo wa mkataba wa NCUC wa kutenganisha
> viti vya GNSO kutoka kwa maeneo, walakini NCUC imekatazwa kuchagua
> wajumbe wake kulingana na SG.
>
> Ungana na NCUC
>
> Mashirika na watu wote binafsi kutoka jamii ya wasio wanabiashara
> wanaalikwa kuungana na NCUC kwenye mpango ya utengenezaji wa sera za
> GNSO ya ICANN. Leta maoni yako kwa mazungumzo ya sera za mtandao wa
> Internet na usaidie kulinda watumizi wa mtandao wasio wa kibiashara
> kwa kushiriki kwa ICANN kupitia kwa NCUC. Ingia leo kwa kwenda hapa:
>
> http://icann-ncuc.ning.com/main/authorization/signUp?
> ---ends----
>
> About Grace:
> =====================================================
> Grace Mutung’u (Bomu) is a young Kenyan lawyer who has been part of
> the Kenya ICT policy process since 2005. She works with theatre
> companies as an actor, marketer and cultural policy advocate. She is
> currently taking a course Intellectual Property Law and the Internet
> at Diplo Online Campus.
>
> Grace is a member of the ICT Consumers Association of Kenya.
> ====================================================
>
-------------- next part --------------
An HTML attachment was scrubbed...
URL: <http://lists.ncuc.org/pipermail/ncuc-discuss/attachments/20090915/f466b5ad/attachment.html>


More information about the Ncuc-discuss mailing list