Kiswahili Language Version of "Top 10 Myths About Civil Society Participation at ICANN"

Alex Gakuru gakuru at GMAIL.COM
Tue Sep 15 21:05:36 CEST 2009


Hi Robin, all,

Grace Muting'u has kindly translated the document into Kiswahili
(spoken by at least 120 million people in East African Community
member countries alone).

Asante (Thanks) Grace.

Regards,

Alex

---begins----
“Porojo Kumi maarufu zaidi  kuhusu uhusikaji wa mashirika ya shirika
la ICANN”, na NCUC

21 Agosti 2009
_____________________________________________________________________________
Porojo ya Kwanza

“Masirika ya kijamii hayatahusika kwenya ICANN chini ya mpango
uliopendekezwa na NCUC.”

Uwongo: Wafanyakazi wa ICANN na wengine wanadai kwamba
mashirika  ya  kijamii hukatwa tamaa yasijihusishe na ICANN
kwa vile mpango uliopendekezwa na ICANN hauhakikishi kwamba
viti katika Kamati ya GNSO vitagawiwa maeneo au washikadau wote.

Ukweli wa mambo ni kwamba uanachama wa NCUC unawakilisha
mashirika 143 yasiyo ya kibiashara pamoja na watu binafsi. Tangu
mwaka 2008 uanachama wa NCUC umeongezeka kwa zaidi ya 215%
- hii ni kwa mujibu wa mwito wa mashirika ya kijamii. Hakuna shirika
hata moja lisilo la kibiashara lililotoa maoni kwamba kuwepo tu kwa
viti vya maeneo katika Kamati ya GNSO ndipo kungewafanya kushiriki
kwenye ICANN. Katika mashirika yaliyotoa maoni yao, hakuna
lilisosema ya kwamba lingeshiriki kwenye ICANN sharti katiba ya
NSCG ingewahakikishia kiti kwenye Kamati ya GNSO.

Porojo ya Pili

“Wengi zaidi kutoka mashirika ya kijamii watashiriki kwenye ICANN
Bodi itakapoingilia”

Picha ya kweli: Kulazimisha kwa Bodi kwa katiba yake au kutosikiliza
kwa Bodi kwa vikundi vya mashirika ya kijamii kutaonekana kama
kukataliwa kwa maoni ya vile vikundi vingi vilivyoonelea kwamba ni hii
ni dhuluma dhidi ya mashirika ya kijamii. Sifa ya ICANN kati ya
mashirika yasiyo ya kibiashara itaharibika kabisa hatua mwafaka
isipochukuliwa au suluhu kupatikana. Hata kama vitendo hivyo
vingekubalika, matokeo  kamili kwa wafanya kazi na kwa katiba
ya NCSG itakuwa kuvinyima nguvu vikundi visivyo vya kibiashara
na kuvifanya hata visipende kushiriki. Kuteuliwa kwa waakilishi na
Bodi hufurutisha  vikundi visivyo vya kibiashara na watu binafsi.
Isitoshe, SIC inayowakilisha maeneo au washika dau wote inahitaji
fedha nyingi sana ambayo mashirika mengi yasiyo ya kibiashara
hayawezi kusimamilia. Pia, mpangilio huo utaleta mgawanyiko kati
ya vikundi huku vikipigania wanachama na kura. Vikundi vingi visivyo
vya kibiashara havitaweza kuingia ICANN GNSO chini ya mpango huo.

Porojo ya Tatu

Kuwepo kwa upinzani kunaweza kupuuzwa tu kama “kampeni ya
uandikaji barua”

Hii ni shutma isiyo ya kweli: Upinzani mkali wa mashirika ya kijamii
kwa katiba ya SIC ulitokea si mara moja bali mara mbili. Pia, kulikuwa
na ongezeko kubwa la wanachama wa NCUC lililotokana na kutopendezwa
kwa jamii yote kwa jumla na vitendo vya wafanyakazi pamoja na Bodi.
Kujaribu kupunguza ushiriki wa mashirika ya kijamii hakutafanikiwa na
kunaonyesha upotovu huu wa hali ya juu. ICANN inahitajika kuwa na
nyakati za maoni ya umma kwa maana ni lazima isikize na kujibu
maswala ya jamii. Maoni ya umma hutokana na kuwepo kwa mawasiliano
na mazungumzo kuhusu hata maswala tata, hata kama ni  miito ya
kuchukua hatua. Hakuna mpango au sheria inayoipa ICANN au
wafanyakazi wake uwezo wa kuamua kutotilia maanani au kupuuza
vikundi karibu vyote vilivyoonyesha kutaka kushiriki kwenye marekebisho
ya GNSO, eti kwa sababu wamewashutumu wafanyakazi wa ICANN.

Jaribio la ICANN la kutaja maoni haya ya muhimu kama “kampeni ya
uandikaji barua” inapuuza ushiriki wa siku zijazo na imani katika
mipango ya ICANN ya kuhusisha umma.

Porojo ya Nne

"Mashirika ya kijamii yamegawanyika kuhusu swala la katiba ya NCSG."

Si Kweli. Hakujawahi kuwa na maoni ya umma yaliyoegemea upande mmoja
kama haya katika historia ya ICANN. Hata kama wafanyikazi wa ICANN
wanaiambia Bodi kwamba mashirika ya kijamii yamegawanyika, maoni zaidi
yanakataa katiba iliyopendekezwa na ICANN na kuiunga mkono
iliyopendekezwa na NCUC. Wanabodi wanaotegemea habari kutoka kwa
wafanyikazi wa ICANN pekee wanaweza kuamini kwamba mashirika ya
kijamii yamegawanyika , lakini wanabodi ambao wanesoma maoni ya umma
wanaweza kuona umoja wa mashirika ya kijamii katika kupinga kulazimishwa
kufanya ICANN inavyotaka.

Porojo ya Tano

"Mashirika ya Kijamii yaliyoko kwa sasa hayawakilishi kamili washikadau wote"

Si kweli kwa vyovyote. Kwa sasa, kikundi cha mashirika ya kijamii,
kijulikanacho
kama NCUC kina wanachama 143 ambao kati yao 73 ni mashirika yasiyo ya
kibiashara na watu banafsi 70 kutoka nchi 48. Hili ni ongezeko la 215% tangu
kanuni  ya uakilishaji wa wote ianzishwe.

Ushiriki wa jamii isiyo ya kibiashara umeongezeka na kwa hivyo si haki kusema
kusema kwamba NCUC haishirikishi washika dau wote bila ya kusema hivyo juu
ya jamii zingine. Hata mwaka wa 2006, utafiti huru uliofanywa na London School
of Economics ulionyesha kuwa NCUC iliwakilisha maeneo mengi zaidi na pia
ilikuwa na watu wengi zaidi tofauti katika kamati ya GNSO wakati wowote, na
kwamba ilibadilisha zaidi wawakilishi wake katika kamati hio ikilinganishwa na
jamii zile zingine sita.

Kwa upande mwingine, jamii ya wanabiashara imekuwa ikiwakilishwa na watu
wale wale 5 kwa Kamati kwa muongo mmoja na kulipokuwa na mwito wa
marekebisho ya GNSO, 3 kati ya wanakamati 6 wa jamii ya kibiashra
watawakilisha Marekani.

Porojo ya Sita

“ALAC inapendelea mkataba uliopendekezwa na wafanyakazi wa ICANN
kuliko ule wa mashirika ya kijamii”

Uwongo: Kiongozi mmoja wa ALAC alisema kuwa anapendelea maktaba
uliopendekezwa na wafanyikazi. Wafanyikazi walichukua msemo huo na
kuupeleka kwa Bodi ya ICANN huku wakidai kwamba ALAC inapendelea
mkataba uliopendekezwa na wafanyikazi wa ICANN. Kwa kweli, taarifa
rasmi iliyotolewa na ALAC na iliyopitishwa na na ALAC ilisema kuwa
wanachama wengi wa ALAC waliunga mkono pendekezo la “kulitenganisha
swala la viti vya Kamati kutoka kwa maeneo ni jambo nzuri na mwelekeo
mwema.”

Porojo ya Saba

"Mkataba wa NCUC utakipa kikundi kile kile kidogo viti 6 badala ya 3"

Uwongo:   Kwa miezi minane iliyopita, NCUC imekuwa ikitangaza kuwa
itajitawanya muda tu NCSG itakapoundwa. Haina maana kuwa na “jamii ya
mashirika yasiyo ya kibiashara” na vile vile “washika dau wasio wa
kibiashara” kwani haya ni maneno yenye maana sawa. Kwa hivyo, viongozi
wa NCUC hawatakuwa na uwezo wa kuendesha NCSG mpya – uongozi mpya
utachaguliwa. Chini ya mkataba, mashirika na watu wote binafsi watapiga
kura kuchaga viti vya Kamati, na si tu wanachama wa hapo mbeleni wa
NCUC. Masharti makali kuhusu uakilishi kutoka maeneo yote ya kijografia
yatamaanisha kuwa wanaowania kutoka maeneo yote duniani
 watachaguliwa hata kama hawatapata wingi wa kura.

Porojo ya Nane

"NCUC haitagawana viti vya Kamati na jamii zingine za mashirika yasiyo
ya kibiashara."

Si Kweli: Mkataba wa NCUC uliundwa ili kuwezesha mashirika yasiyo ya
kibiashara kuwa na wawaniaji wao wa viti vya Kamati. Ikilinganishwa na
uwepo na uanachama wa NCUC, jamii nyingi zenye ajenda zinazoshindana
zitajitokeza. Kukua kwa maeneo kutoka mashinani hadi juu ni bora
kuliko mwelekeo wa Bodi/Wafanyikazi- pia unafanana zaidi na mapedekezo
ya BGC. Maktaba wa SIC unaelekeza uundaji wa maeneo kutoka juu na hii
ni ngumu na inaipa Bodi uwezo uliozidi kuamua “ushirikishaji” au
 “umuhimu” wa washiriki wapya. Kwa vile uakilishi wa maeneo unategemea
viti vya Kamati. Viti vya Kamati vikilinganishwa na maeneo, kila eneo
litakuwa na mivurutano kuhusu kupewa kwa viti hivi vya Kamati

Porojo ya Tisa

"NCUC inataka kunyakua haki ya Bodi ya kupitisha maeneo”

Uwongo: Watu wanaosema hivi ni dhahiri ya kwamba hawajasoma mkataba
uliopendekezwa na NCUC. NCUC inapendekeza kwambo Bodi iwe na uwezo wa
kupitisha au kukataza maeneo mapya yaliyoundwa chini ya mkataba huo.

Pendekezo letu ni kuwe na na mielekezo ya kufuatwa (k.m nambari ya
wagombea) kwa kuundwa kwa maeneo mapya halafu mapendekezo
yatumwe kwa Bodi. Dhana ilikuwa kupunguza mzigo wa uundaji wa maeneo mapya kwa
wagombea na pia kwa Bodi.

Mkataba uliopendekezwa na NCUC una mapendekezo rahisi sana ya kuunda
maeneo mapya ukilinganishwa na ule wa SIC ambao utafanya uundaji wa
maeneo mapya kuwa jambo gumu sana.

Porojo ya Kumi

“Azma ya kuwa na eneo ni kuwa na kiti kwenya Kamati ya  GNSO.”

Uwongo:  wengine hudai kwamba viti vya Kamati ya GNSO lazima
vilinganishwe kikamili na maeneo haswa kwa vile eneo halina maana bila
kuhakikishiwa kiti kwenye Kamati ya GNSO. Lakini, kusema hivyo ni
kutoelewa umuhimu wa maeneo katika GNSO mpya, ambao ni kuwapa sauti na
namna ya kushiriki katika utengenezaji wa sera –wala si kuhakikishiwa
kuwa na mjumbe asiye hata na mori wa kuafikiana na maeneo mengine.

Viwili kati ya vikundi vitatu vya washikadau (Registries and Registrars)
vilipitisha mwelekeo wa mkataba wa NCUC wa kutenganisha
viti vya GNSO kutoka kwa maeneo, walakini NCUC imekatazwa kuchagua
wajumbe wake kulingana na SG.

Ungana na NCUC

Mashirika na watu wote binafsi kutoka jamii ya wasio wanabiashara
wanaalikwa kuungana na NCUC kwenye mpango ya utengenezaji wa sera za
GNSO ya ICANN. Leta maoni yako kwa mazungumzo ya sera za mtandao wa
Internet na usaidie kulinda watumizi wa mtandao wasio wa kibiashara
kwa kushiriki kwa ICANN kupitia kwa NCUC. Ingia leo kwa kwenda hapa:

http://icann-ncuc.ning.com/main/authorization/signUp?
---ends----

About Grace:
=====================================================
Grace Mutung’u (Bomu) is a young Kenyan lawyer who has been part of
the Kenya ICT policy process since 2005. She works with theatre
companies as an actor, marketer and cultural policy advocate. She is
currently taking a course Intellectual Property Law and the Internet
at Diplo Online Campus.

Grace is a member of the ICT Consumers Association of Kenya.
====================================================
-------------- next part --------------
A non-text attachment was scrubbed...
Name: grace mutungu.jpg
Type: image/jpeg
Size: 7792 bytes
Desc: not available
URL: <http://lists.ncuc.org/pipermail/ncuc-discuss/attachments/20090915/cad90ca9/attachment.jpg>


More information about the Ncuc-discuss mailing list